MIA — Computer Application

Syllabus Kamili (Wiki 6)

Kozi maalum kwa wanaoanza kutoka zero: kompyuta msingi, Microsoft Word, na Microsoft Excel.

Ratiba & Njia ya Kusoma

  • Muda: Wiki 6
  • Online: Video kwenye Student Portal + msaada WhatsApp
  • Physical (hiari): Physical (hiari): uje mahali pale unapokuwa na muda wa bure — Alhamisi, Ijumaa, Jumamosi & Jumanne kuanzia saa 5:00 jioni
  • Mahali: Magari saba, karibu na St. Joseph University — Dar es Salaam
  • Mahali: Magari saba, karibu na St. Joseph University — Dar es Salaam. Hakuna ratiba ngumu — fika ukiwa na muda wako wa bure kwa msaada wa ana kwa ana.
  • Masaa: Takriban masaa 4–6 kwa wiki (online + physical ikiwa unapatikana)

Ada ya Mafunzo

Kiasi kamili: TSH 50,000

Malipo: TSH 25,000 kabla ya kuanza, halafu TSH 25,000 katikati — au lipa yote mara moja.

Tigo Pesa Lipa Namba: 43527093IMANI MUSTAFA HUSSEIN

WhatsApp baada ya malipo: +255 673 893 640

Mchakato wa Wiki kwa Wiki

Wiki 1: Msingi wa Kompyuta

Mada:

  • Kompyuta ni nini, sehemu za hardware (screen, keyboard, mouse)
  • Kuwasha/kuzima kompyuta kwa usalama
  • Desktop, taskbar, Start menu
  • Kufungua na kufunga programu

Kazi ya vitendo: Fanya mazoezi ya kufungua Chrome, Notepad, na kuzima programu kwa mpangilio.

Wiki 2: Files, Folders & Internet

Mada:

  • Kutengeneza folders na files
  • Kuhifadhi, kupata, na kukopi faili
  • USB / Google Drive (msingi)
  • Chrome: kutafuta, bookmarks, downloads
  • Kutuma faili kwa WhatsApp / Email

Kazi ya vitendo: Tengeneza folder ya masomo yako na uhifadhi document 3 tofauti ndani yake.

Wiki 3: Microsoft Word — Msingi

Mada:

  • Kufungua Word na kuunda document mpya
  • Kuandika, kuhariri, font, bold, italic, underline
  • Paragraph alignment, spacing, bullets & numbering
  • Kuhifadhi na kuchapisha (Print / PDF)

Kazi ya vitendo: Andika barua rasmi ya chuo au kazi (1–2 kurasa) kwa muundo sahihi.

Wiki 4: Microsoft Word — Kazi za Chuo/Kazi

Mada:

  • Headers, footers, page numbers
  • Tables na borders
  • Insert picha na resize
  • Templates: CV / cover letter (msingi)

Kazi ya vitendo: Tengeneza report ya masomo yenye jedwali na picha angalau moja.

Wiki 5: Microsoft Excel — Msingi

Mada:

  • Cells, rows, columns
  • Kuandika data na formatting
  • Formulas za msingi: SUM, AVERAGE, COUNT
  • Charts (msingi)

Kazi ya vitendo: Tengeneza jedwali la matumizi ya pesa ya mwezi na hesabu jumla kiotomatiki.

Wiki 6: Microsoft Excel — Vitendo & Mwisho

Mada:

  • Sorting na filtering data
  • IF formula (msingi)
  • Budget / attendance sheet za vitendo
  • Mapitio ya mwisho + tathmini ya kozi

Kazi ya vitendo: Tengeneza Excel sheet ya matokeo au budget inayotumia formulas 3+.

Apply for Computer ApplicationBack to Academy